Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Wednesday 9 January 2013

Wazayuni waifanya misikiti kuwa masinagogi

Walowezi wa Kizayuni wameubadilisha msikiti mmoja wa kihistoria ulioko Baitul Muqaddas na kuufanya Sinagogi. Taasisi ya Wakfu na Turathi za Kihistoria ya al Aqsa imetangaza leo kuwa, walowezi wa Kizayuni wameushambulia Msikiti wa kihistoria wa Hadhrat Daud AS huko Baitul Muqaddas na kuiharibu vibaya sehemu moja ya msikiti huo na sehemu iliyobaki imefanywa maabadi ya Mayahudi. Taasisi hiyo imeeleza kuwa, wiki iliyopita walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali wakisimamiwa na askari wa wa Israel waliushambulia na kuuharibu msikiti mwingine wa kihistoria uliojengwa katika karne ya 17 katika eneo la Aal Adajani huko kusini magharibi mwa Masjidul Aqswa na ghorofa ya kwanza ya msikiti huo imefanywa Sinagogi. Taasisi hiyo imeeleza kuwa, vitendo hivyo vya walowezi wa Kiyazuni ni sehemu ya siasa za kutaka kuliyahudisha eneo lote la Baitul Muqaddas kwa kufuta kabisa sura ya Kiislamu katika mji huo.
Takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Wakfu na Turathi za Kihistoria ya al Aqswa zinaonesha kuwa, tokea utawala wa Kizayuni wa Israel ulipoanza kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina kwa lengo la kuziyahudisha, umeharibu zaidi ya misikiti elfu moja.

0 comments:

Post a Comment