Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Wednesday 9 January 2013

Mahakama ya Venezuela: Chavez ataapishwa baadaye

Mahakama Kuu ya Venezuela imesema kwamba, kuakhirisha zoezi la kuapishwa Rais Hugo Chavez wa nchi hiyo ni jambo halali, na kwamba serikali iliyoko madarakani iendelee kuongoza nchi hadi atakapoapishwa.
Mahakama hiyo imeongeza kuwa, Rais huyo anaweza kula kiapo wakati wowote baada ya leo Januari 10, lakini pia imetaka afanyiwe vipimo kabla ya sherehe za kuapishwa kutokana na hali yake ya kiafya.
Hukumu hiyo imetangazwa baada ya makundi ya wapinzani kutaka mahakama hiyo ya kilele itoe uamuzi juu ya hali ya Rais huyo anayesumbuliwa na maradhi ya kansa. Kiongozi wa mrengo wa upinzani wa Venezuela Hemrique Capriles amekubali uamuzi huo wa mahakama lakini amesema kwamba unafunika baadhi ya mambo.
Chavez aliingia mara ya kwanza madarakani mwaka 1999 na kuchaguliwa tena kuingoza Venezulea kwa miaka mingine 6 Oktoba mwaka jana. Mwezi mmoja kabla ya kuwadia muda wa kuapishwa alifanyiwa operesheni kutokana na maradhi ya kansa yanayomsumbua.

0 comments:

Post a Comment