Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 18 October 2012

MAONI YANGU KUHUSU KUULIWA KWA ASKARI POLISI-ZANZIBAR.


Uislam haujahalalisha damu ya MUUMINI kumwagwa na wala muumini hajahalalishiwa kuimwaga damu ya muumini mwenzake.Na inapotokea mtu akamwaga damu ya mwenzake na ni katika nchi yenye kutekeleza sheria ya kiislam,basi mtu huyo lazima na yeye auwawe ili kuondoa chuki na fitna kwa wale waliouliwa mtu wao.

Kwa jambo lililofanyika la kumuuwa huyo askari naweza kusema hili si la halali na si katika matendo ya watu wenye imani ya kweli,lakini kwa upande mwengine tujiulize,,kwanini askari huyu tu ndie alieuwawa, tena kwa ghafla?????Akili yangu inaniambia kuwa,,kuuliwa kwa huyu askari kunahitaji uchunguzi wa hali ya juu,maana watu wenye akili zao na imani zao,hawawezi tu kutoka walikotoka wakaenda moja kwa moja kumuuwa huyu askari,inawezekana na yeye alikuwa katika harakati fulani fulani........................


Tuchukulie mfano mmoja tu,2001 kisiwani PEMBA, mambo waliyofanyiwa wazee wetu na mama zetu na hao hao askari, mengine hata hayasemeki,na WALLAH wengine walikuwa ni WAZANZIBAR wenzetu( MKUU WA KITUO CHA POLISI CHA KASKAZINI PEMBA.), na kwa bahati nzuri sisi nyumbani waliweza hata kuingia mpaka ndani(BAADA YA KUVUNJA MLANGO),tukawa na uwezo wa kuwasikia lafdhi zao,kwa kweli ni waznz wenzetu,watu wa bara walikuwa wachache,japo walikuwepo.

Sasa haya yote yalitendeka lakini tokea kipindi hicho sijawahi kusikia askari kachinjwa na kuuliwa,na hao askari wapo mpaka leo.SASA KWANINI AWE NI ASKARI HUYU TU tena katika jimbo la bububu ambalo hivi karibuni tu yalitokea machafuko ambayo yalipelekea majeraha makubwa kwa watu?


Mimi nafikiri kuna kundi maalum ambalo hujiingiza katika vurugu kama hizi ilimradi tu kile kinachopiganiwa kisipatikane.Nanukuu kauli ya shkh MSELLEM aliposema"KATIKA MSAFARA WA MAMBA,NA KENGE WAMO" .Na inawezekana wao ndio waliosababisha kifo cha askari huyu.(MUNGU AMSAMEHE MAKOSA YAKE).

Kwa hivyo ndugu zangu nawashauri,sio kila baya linalotendeka katika harakati zilizopo sasa,tusikurupuke tu na kusema kwamba waliofanya hivyo ni UAMSHO ama ni WAISLAM.Siwezi kuamini kuwa wanaovunja BAA na MADUKA ya watu wakaiba kila kitu na kufikia hatua ya kunywa POMBE,wote hawa ni uamsho au ni waislam!!!!!

LAZIMA TUFIKIRIE MARA MBILIMBILI KABLA YA KUTOA MAAMUZI KATIKA AKILI ZETU.muumini wa kweli,mambo kama haya hawezi kufanya.

NAPENDA KUWAPA POLE WALE WALIOFIKWA NA MSIBA HUU,NA NAPENDA KUISHAURI SERIKALI YA ZANZIBAR,KAMA KWELI WAO HAWAHUSIKI NA JAMBO HILI LA KUTEKWA NYARA KIONGOZI WA UAMSHO,BASI NI VYEMA KUCHUKUWA HATUA ZA HARAKA KATIKA KUPATIKANA KWAKE ILI KUONDOA FIKRA MBAYA KWA WANANCHI WAO.
SERIKALI INATAKIWA IELEWE KUWA,HUYU NAE NI RAIA NA ANA KILA HAKI YA KULINDWA KAMA ANAVYOLINDWA RAIS.NA WAELEWE KUWA BAYA LOLOTE LITAKALOTOKEA KWAKE(KAMA NI KIFO AU KUTOKUONEKANA TENA,MUNGU AMUHIFADHI) BASI NCHI HAITOKUWA NA AMANI TENA NA WALA WANANCHI HAWATOKUWA NA IMANI TENA NA VIONGOZI WAO(Allah anusuru tusifike huko)

Hivi tujaalie kama alietekwa ni KATIBU MKUU WA CCM-ZANZIBAR,hali ya viongozi wetu ingekuwaje?wangelinyamaza na kusema kuwa,wanafuatilia?Mi nafikiri wangelikwishachukuwa hatua za haraka,hata kukodi majeshi kutoka nje ya ZNZ ili apatikane,sasa wawili hawa wana tofauti gani katika sheria na ulinzi?
Natumai viongozi wetu ni waelewa na wasikivu.
WABILLAH ATAWFIQ.

0 comments:

Post a Comment