Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 4 July 2013

Serikali na wapinzani wa Guinea wakubaliana




Serikali ya Guinea Conakry na vyama vya upinzani wameafikiana juu ya kufanyika uchaguzi wa Bunge uliocheleweshwa kwa muda mrefu, mwishoni mwa mwezi Septemba, ili kuhitimisha kipindi cha mpito.
Mauktar Diallo ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa upinzani amesema, wamefikia makubaliano hayo na kwamba ana matumaini jamii ya kimataifa pia itahakikisha yanatekelezwa. Diallo ameongeza kwamba, makubaliano hayo yanamaanisha kuwa, uchaguzi wa Bunge utafanyika baada ya siku 83 tarehe 29 Septemba mwaka huu.
Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Juni 30 lakini uliakhirishwa baada ya wimbi la maandamano ya wapinzani waliokuwa wakimtuhumu Rais Alpha Conde kuwa ana mpango wa kuiba kura.

0 comments:

Post a Comment