Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 4 July 2013

Bustani ya Gezi, wapinzani waishinda serikali Uturuki




Mahakama ya Uturuki imefuta mpango wa serikali wa kubomolewa bustani iliyo karibu na Medani ya Taksim mjini Istanbul, suala lililozusha maandamano ya kupinga serikali nchini humo.
Uamuzi wa mahakama hiyo unaonekana kuwa pigo kwa Waziri Mkuu Racep Tayyip Erdogan aliyekuwa aking'ang'ania mpango huo, na unaonekana kuwa ushindi kwa wapinzani waliokuwa wakiupinga.
Tangu Mei 31 Istanbul imekuwa ikishuhudia maandamano ya kupinga serikali huku polisi wakikabiliana na waandamanaji waliokuwa wamepiga kambi katika Medani ya Taksim kupinga uamuzi wa kubomolewa bustani ya Gezi. Bustani hiyo imezoeleka kuwa eneo la mijumuiko, mikusanyiko na maandamano na pia kivutio cha watalii huku ikiwa ni sehemu pekee ya kijani ya umma iliyobakia kwenye mji wa Istanbul na serikali ilitaka kuibomoa kujenga maduka.

0 comments:

Post a Comment