Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday 1 July 2013

Obama kuwasili leo jijini Dar es Salaam, Tanzania

                               22 shaaban,1434 Hijiriyah/ 01 july,2013 Miyladiyah
Rais Barack Obama wa Marekani, anatarajia kuwasili saa nane mchana nchini Tanzani kwa ziara rasmi ya siku mbili. Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizotembelewa tayari na Rais Obama. Hata hivyo wananchi wengi wa Tanzania wamelalamikia safari hiyo, kutokana na kuzorota shughuli zao za kijamii kwa muda wa wiki moja sasa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Obama anayeongozana na familia yake anatarajiwa kupokelewa jijini Dar es Salaam na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete na baadaye kwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi. Hapo juzi polisi nchini Afrika Kusini walipambana na waandamanaji waliokuwa na hasira ambao waliteketeza moto picha za rais huyo wa Marekani alipokuwa safarini nchini humo. Waandamanaji hao pia waliteketeza moto bendera za Marekani katika maandamano hayo yaliyofanyika nje ya Chuo Kikuu cha Johannesburg, tawi la Soweto, sehemu ambayo Obama aliwahutubia wanafunzi. Akiwa nchini Senegal Rais Macky Sall wa nchi hiyo alimwambia kinagaubaga Obama kuwa, nchi yake haiko tayari kuruhusu ushoga na maingiliano ya ngono kati ya watu wa jinsia moja.

0 comments:

Post a Comment