Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday 1 July 2013

Jeshi la Misri lakadhibisha madai ya mapinduzi


Jeshi la Misri limetangaza kuwa, taarifa iliyotolewa jana kwa makundi ya kisiasa ya kuyataka yafikie  mwafaka, haina maana ya kutaka kufanya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.
Jeshi la Misri limeeleza kuwa, taarifa hiyo imetolewa kwa  lengo la kuyashinikiza makundi ya kisiasa na wanasiasa nchini humo kufikia mwafaka na serikali ya Cairo. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, iwapo wanasiasa wa Misri watashindwa kufikia mwafaka na kutekeleza matakwa ya wananchi katika kipindi cha masaa 48 yajayo, litalazimika kuingilia kati kwa shabaha ya kutatua mgogoro huo.
Wakati huohuo, masaa machache baada ya jeshi kutoa muda wa masaa 48 ya kutatuliwa mgogoro wa Misri, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Misri Muhammad Kamil Amr ametangaza kujiuzulu, baada ya kushadidi maandamano ya wapinzani wa Rais Morsi. Hadi sasa mawaziri 10 na magavana watatu wa serikali ya Misri wameshajiuzulu. Vilevile mshauri wa masuala ya kijeshi wa Rais Morsi naye alitangaza kujiuzulu hapo jana.


0 comments:

Post a Comment