Wizara ya
Ulinzi ya Kenya imekanusha tuhuma kwamba jeshi la nchi hiyo linachochea
machafuko katika mji wa Kismayo, Kusini mwa Somalia. Taarifa ya wizara hiyo
imesema jeshi la Kenya linafanya juu chini kuona amani na utulivu vinarejea
Somalia. Serikali ya Somalia imelituhumu jeshi la Kenya kwamba limeshindwa
kufanya kazi barabara na hivyo kusababisha mapigano ya hivi karibuni kati ya
makundi tofauti yaliyosababisha vifo vya watu 65. Serikali ya Mogadishu
imeuandikia barua Umoja wa Afrika ikisema Kenya imekuwa ikiegemea upande mmoja
na kulipendelea kundi moja dhidi ya makundi mengine na ilimkamata afisa mmoja
mkuu wa jeshi la Somalia akitumia silaha nzito katika maeneo ya raia katika
eneo la Kismayo, kusini mwa Somalia. Kenya ina kikosi chake kusini mwa Somalia
karibu na mpaka wake kama sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda
amani. Somalia imekuwa katika vita kwa miongo kadhaa sasa lakini matumaini
yalikuwa kwamba kikosi cha Umoja wa Afrika wakiwemo wanajeshi wa Kenya wataleta
tofauti kubwa katika nchi hiyo. Sasa Somalia inautaka Umoja wa Afrika
kuchunguza madai hayo na iwapo yatabainika kuwa ya kweli basi jeshi la Kenya
liondolewe nchini humo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment