Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 4 July 2013

JWTZ: Njooni Sabasaba muone tunachokifanya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limewataka wananchi wanaotembelea maonyesho ya kimataifa ya biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kutembelea banda lao ili kujifunza kazi mbalimbali wanazofanya.


Hali kadhalika, limewataka Watanzania kuweka uzalendo kwanza kwenye kila jambo ili kuijenga Tanzania kwa ajili yao.


Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na NIPASHE kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere katika maonyesho hayo yaliyojumuisha washiriki 1,341 kutoka nchi 32.


Alisema uzalendo ndiyo nyenzo pekee ya kulijenga Taifa na kutokukubali kutumiwa na mamluki wa ndani na nje wanaolitazama Taifa kwa jicho la husda.


"Tunawakaribisha Watanzania kufika kwenye banda hili kujifunza mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwaona makomandoo na jinsi Jeshi lilivyo na wataalam katika sekta zote ambao kipindi cha amani hutumika kufanya shughuli za maendeleo kama afya na ujenzi wa madaraja," alisema Kanali Mgawe.


Alisema matarajio ya wananchi wengi wanaofika kwenye banda hilo ni kuona silaha na zana mbalimbali zinazotumika wakati wa vita.


Kanali Mgawe aliongeza kuwa lengo la kushiriki maonyesho hayo ni kueleza kazi za Jeshi na kubadili mtazamo hasi kwa wananchi wawaone ni raia wa kawaida.

 

0 comments:

Post a Comment