Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 1 July 2013

Assad apiga marufuku utumiaji wa watoto vitani


Rais Bashar al Assad wa Syria amepiga marufuku utumiwaji watoto kwenye operesheni za kijeshi na kusisitiza kuwa watakaopatikana na hatia ya kuwatumia watoto hao watakabiliwa na adhabu kali ya kifungo jela.
Rais Assad ameongeza kuwa, mtu yeyote atakayethubutu kuwashirikisha vijana walio na umri wa chini ya miaka 18 kwenye oparesheni za kijeshi na masuala yanayofungamana nayo kama kubeba silaha, zana za kijeshi na kutega mada za milipuko kwenye vituo vya ukaguzi na maeneo mengineyo watakabiliwa na kifungo cha kuanzia mwaka mmoja hadi 10 jela na kulipa faini ya lira milioni tatu.
Rais wa Syria ameongeza kuwa, adhabu ya kifungo cha maisha itatolewa kwa watu ambao watapatikana na hatia ya kuwalazimisha watoto kubeba mada za milipuko na iwapo watoto hao watauawa, basi wahusika  watakabiliwa na adhabu ya kifo.

0 comments:

Post a Comment