Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 4 July 2013

AGRA yakunwa `mapinduziya kijani` nchini Tanzania
 Upatikanaji mbegu bora za mahindi, mtama na alizeti, unaifanya Tanzania kupiga hatua katika kuelekea azma ya kufikia mapinduzi ya kijani katika sekta ya kilimo nchini.

Hali hiyo pamoja na mambo mengine, itaboresha na kuwezesha upatikanaji wa chakula cha uhakika kwa wakazi wa maeneo tofauti ya nchi.

Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa na taasisi inayohimiza mapinduzi ya kijani barani Afrika (AGRA), ambayo Mwenyekiti wake ni Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN), Koffi Annan.

Kwa mujibu wa AGRA, wadau na kampuni zinazojishughulisha katika sekta kilimo nchini, wamefikia kiwango kizuri cha kuzalisha mbegu bora za mahindi, mtama na alizeti, hivyo kuielekea azma ya kuyafikia mapinduzi ya kijani.

Akizungumza mjini Arusha, Ofisa  wa AGRA anayeshughulika na program ya mfumo wa mbegu Afrika (Pass), Dk. George Bigirwa, alisema upatikanaji wa mbegu bora ni moja ya hatua muhimu katika kufikia ndoto ya kuwa mapinduzi ya kijani katika kilimo.

Dk. Bigirwa, akiwa na Makamu wa Rais wa program ya Pass, Dk. Segenet Kelemu, walitembelea miradi inayofadhiliwa na AGRA katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo alisisitiza kuwa wakulima wengi wameanza kunufaika kupitia mradi wa mbegu bora.

Kwa mujibu wa Dk. Bigirwa, kampuni 11 za Tanzania zimepiga hatia kubwa katika uzalishaji wa mbegu bora na zenye ufanisi mkubwa shambani, ikiwa ni miongoni mwa matokeo ya ufadhili wa AGRA.

Kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2007 hadi sasa, AGRA imeshatumia takribani dola 11,084,733 kwa ajili ya mradi wa mbegu bora kupitia mpango wa Pass.

Tafiti zinaonyesha kuwa uwapo wa mbegu bora zinazozalishwa nchini, kunachangia kuokoa fedha za kigeni ambazo zingetumika kununua bidhaa hiyo nje ya nchi.

Program ya Pass inasaidia makundi ya wanaozalisha mbegu wanaofanya kazi kwa karibu na wakulima, kupata aina mpya ya mbegu zenye ubora wa hali ya juu na zenye tija inayotakiwa.


0 comments:

Post a Comment