Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 1 June 2013

Wengi wafaulu kidato cha sita

                           22Rajab,1434 Hijiriyah/ JUNY 01,2013 Miyladiyah
 Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde akitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2013, kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis Felix 

 Baraza la Mitihani Nchini (Necta), limetangaza matokeo ya kidato cha sita ambapo asilimia 87.85 wamefaulu huku kundi la shule 20 za mwisho likitawaliwa na shule kongwe nchini na zile za Zanzibar.
Akitangaza matokeo hayo jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde, alisema watahiniwa 50,611 walifanya mtihani huo na kati yao 44,366 sawa na asilimia 87.85, wamefaulu.
Mwaka 2012 wanafunzi waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 46,658 sawa na asilimia 87.65.
Watahiniwa wa shule
Dk Msonde alisema kuwa, watahiniwa wa shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya waliofanya mtihani huo.
“Wasichana waliofaulu ni 13,286 sawa na asilimia 95.80 na wavulana 26,956 sawa na asilimia 93.03,” alisema.
Mwaka 2012 watahiniwa 40,775 sawa na asilimia 92.30 walifaulu mtihani huo.
Watahiniwa wa kujitegemea
Alisema kuwa, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo walikuwa ni 7,659 na waliofaulu ni 4,124 sawa na asilimia 53.87.
Ufaulu katika kundi hili umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 5,883 sawa na asilimia 64.96 ya wote waliofanya mitihani hiyo.
Ufaulu kwa madaraja
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, watahiniwa 325 sawa na asilimia 0.76 ya wote waliofanya mtihani huo walipata daraja la kwanza, kati yao wavulana wakiwa ni 188 sawa na asilimia 0.65 na wasichana 137 sawa na asilimia 0.99.

0 comments:

Post a Comment