Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 22 June 2013

Wapinzani wa Sudan waitisha serikali

                             
Muungano wa vyama vya upinzani nchini Sudan umetishia kuanzisha harakati za siri dhidi ya serikali.

Muhammad Dhiyaaudeen msemaji rasmi wa Chama cha Kisoshalisti cha al-Baath amesema katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti moja kwamba, endapo serikali ya Khartoum itaendelea na hatua zake za kuwabana wapinzani, mrengo huo wa upinzani utaweka kando njia za amani na badala yake utatumia mabavu dhidi ya serikali jambo ambalo litasababisha maafa.
 Kiongozi huyo mwandamizi wa muungano wa wapinzani nchini Sudan ameashiria mpango wa siku mia moja wa wapinzani wa kuiangusha serikali ya nchi hiyo na kusema kwamba, mpango huo umekibana chama tawala na kuonesha wazi udhaifu wa mfumo unaotawala nchini Sudan. 
Vilevile amezikosoa vikali sera za serikali na kusisitiza kwamba, sera hizo zimewafanya wananchi wa Sudan kuwa miongoni mwa watu masikini zaidi duniani.

 
 

0 comments:

Post a Comment