Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 25 June 2013

Vitambulisho vya Taifa Dar vyaiva

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) itaanza kutoa vitambulisho kwa wananchi wa kawaida wa Mkoa wa Dar es Salaam, kutokana na zoezi la uandaaji wa vitambulisho hivyo kuwa katika hatua za mwisho.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati cha Nida, Thomas William, alipokuwa akizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam.

William alisema wananchi watatakiwa kwenda kuweka picha na alama ya dole gumba katika Serikali za Mitaa yao kwani taarifa zao kamili zipo katika uongozi wa mitaa yao.

Pia alisema kuwa vitambulisho hivyo vitatumika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka ni na baadaye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Zoezi la ugawaji vitambulisho limeanzia kanda ya Mashariki na watumishi wa umma 220,000 wamekwishapatiwa vitambulisho hivyo na jumla ya wakazi wapatao milioni tatu wa Mkoa wa Dar es Salaam watapatiwa vitambulisho hivyo.

Zoezi la usajili wa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya taifa ulikamilika katika Mkoa wa Dar es Salaam Julai mwaka jana. Lengo la Nida ni kutaka kila Mtanzania anapatiwa kitambilicho cha taifa na kukitumia katika uchaguzi wa 2015


0 comments:

Post a Comment