Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 22 June 2013

Russia yapiga marufuku Hijab shuleni na vyuoni

                                
 
Uvaaji wa hijabu na nguo nyingine zenye kuonyesha nembo ya kidini umepigwa marufuku kwenye mashule na vyuo vikuu vya kusini mwa  Russia. 

Gavana wa Jimbo la Astrakhan nchini Russia amesema kuwa, kuanzia mwezi Septemba mwaka huu  ni marufuku kuvaa mavazi yenye kuonyesha nembo ya kidini kwenye shule na vyuo vikuu vilivyoko katika jimbo hilo. 

Ameongeza kuwa, Russia ni nchi ya kisekula, hivyo inapasa kukabiliana na baadhi ya makundi ya kikabila na kidini yanayotaka kudhihirisha  itikadi na imani zao kwenye taasisi za elimu katika eneo hilo. 

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012, asilimia 46 ya wananchi wa jimbo la Astrakhan ni Wakristo wa Madhehebu ya Orthodox, asilimia 16 ni Waislamu na iliyosalia ni wafuasi wa dini na madhehebu nyinginezo.

0 comments:

Post a Comment