Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 22 June 2013

Rais Morsi asisitiza mazungumzo Misri

                            
  Rais Mohammad Morsi wa Misri kwa mara nyingine tena ametoa wito wa kufanyika mazungumzo na upinzani ili kupunguza mgogoro wa kisiasa nchini humo kabla ya kufanyika maandamano makubwa yaliyoitishwa na wapinzani wake Juni 30.
Katika mahojiano na gazeti la Akhbar al-Youm, Morsi amesema vyama vyote vya kisasa vinapaswa kukaa pamoja na kujadili njia za kumaliza mgogoro uliopo kwa maslahi ya taifa. Wito huo wa Morsi umetolewa siku moja baada ya maelfu ya wafuasi wake kujitokeza katika mji wa Cairo siku ya Ijumaa na kutangaza kumuunga mkono.
Wapinzani wamepanga kuitisha maandamano makubwa Juni 30 kwa lengo la kumtaka rais Morsi ajiuzulu na uchaguzi wa mapema wa rais uitishwe.
Kiongozi mwandamizi wa upinzani Mohammad Al Baradei ametoa wito kwa Rais Morsi ajiuzulu kabla ya maandamano ya wapinzani. 
Aidha amesema mapinduzi ya wananchi wa Misri yametokomezwa na kwamba Wamisri wanapaswa kumiminika tena mitaani kwa ajili ya kudumisha mapinduzi yao.

0 comments:

Post a Comment