Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 4 June 2013

Raia wa kigeni 27 wahukumiwa nchini Misri

                                 

 Mahakama ya Cairo Jana imewahukumu bila kuwepo mahakamani, raia wa kigeni wapatao 27 wakiwamo Wamarekani 16 kwa tuhuma za kutoa misaada ya kifedha kwa taasisi tofauti za nchi hiyo, kinyume cha sheria. Ripoti zinasema kuwa, watuhumiwa hao wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela. Kabla ya hapo serikali ya Cairo, ilikuwa imetangaza kuwahukumu raia wa kigeni 44 wakiwamo Wamarekani 19, kwa tuhuma za kuzisaidia taasisi binafsi za nchi hiyo, kinyume cha sheria. Kwa mujibu wa serikali ya Misri, watuhumiwa hao ni raia wa Ujerumani, Marekani, Norway, Serbia, Jordan na Palestina. Habari zinasema kuwa, raia hao wa kigeni waliingi kinyemela nchini humo, wakati wa kujiri mapinduzi ya wananchi dhidi ya utawala wa dikteta Hosni Mubarak, kwa lengo la kuzusha fitina nchini.

0 comments:

Post a Comment