Huku maandamano makubwa yakiwa bado yanaendelea dhidi ya serikali ya
Uturuki, mamia ya waandamanaji leo wamefanya maandamano mbele ya ofisi
ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Receb Tayyip Erdogan. Waandamanaji hao
waliokuwa wamejawa na hasira, wamekabiliana vikali na polisi katika eneo
hilo. Machafuko hayo yaliyoanza siku ya Alkhamisi iliyopita mjini
Istanbul na kuenea karibu maeneo yote ya Uturuki, yamesababisha watu
kadhaa kuuawa huku zaidi ya wangine 200 wakijeruhiwa na maelfu kutiwa
mbaroni. Hii ni katika hali ambayo, jumuiya ya wafanyakazi nchini humo,
imetangaza mgomo wa siku mbili wa wafanyakazi kuanzia leo, kulalamikia
ukandamizaji wa kufurutu mipaka unaofanywa na serikali dhidi ya
waandamanaji. Wakati huo huo ofisi za ndege nchini Uingereza na Italia,
zimetangaza kupunguza asilimia 30 ya safari za kitalii nchini Uturuki.
Sekta ya utalii huiingizia nchi hiyo fedha nyingi za kigeni, ambapo kwa
mwaka serikali ya Ankara hupata kiasi cha dola bilioni 22. Maandamano ya
kupinga serikali ya nchi hiyo yameendelea katika miji ya Istanbul,
Ankara, Izmir, Mugla na Antalya.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment