Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 27 June 2013

Obama awasili Senegal na kukutana na Macky Sall

Rais Barack Obama wa Marekani ambaye ameanza safari yake ya kulitembelea bara la Afrika leo amekutana na mwenzake wa Senegal Macky Sall. 
Katika mazungumzo hayo Obama amesifia hatua alizozitaja kuwa za kushangaza za kuimarisha demokrasia zilizopigwa na nchi za bara la Afrika. 
Ameongeza kuwa, Senegal ni moja ya waitifaki wenye nguvu zaidi wa Marekani barani humo na kwamba nchi hiyo inaelekea kuwa mfano mzuri wa utawala bora. 
Hii ni safari ya 3 ya Obama barani Afrika ambako atazitembelea pia nchi za Afrika Kusini na Tanzania. 
Obama amesema kuwa, ijapokuwa hali ya Mandela si nzuri lakini hatovunja safari yake ya Afrika Kusini na kuongeza kwamba lolote lile litakalotokea Mandela ataendelea kukumbukwa kama shujaa kutokana na mema aliyoyafanya. Katika ziara yake hiyo nchini Senegal pamoja na mambo mengine Obama na mkewe wanatarajiwa kutembelea kisiwa cha Goree, ambacho kilikuwa kituo cha kusafirishia watumbwa katika pwani ya mji mkuu Dakar.  
 

0 comments:

Post a Comment