Wagombea 21
wa nafasi ya urais nchini Madagascar wamewataka wagombea watatu wa
kinyang'anyiro hicho wajiengue kwenye mbio za urais nchini humo.
Wagombea hao
21 kati ya 41 wametangaza kuwa, hawatashiriki kwenye vikao vya uchaguzi wa rais
hadi pale watakapojiondoa wagombea watatu ambao ni Lalao Ravalomanana, mke wa
Marc Ravalomanana Rais wa zamani wa nchi hiyo, Andry Rajoelina Rais wa serikali
ya mpito, na Didier Ratsiraka rais wa zamani wa nchi hiyo.
Jean Lahiniriko
mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya rais katika uchaguzi ujao nchini humo
amesema kuwa, kushiriki kwenye vikao hivyo ina maana ya kuunga mkono ushiriki
wa wagombea hao.
Wagombea hao watatu walipuuza takwa lililotolewa na wakuu wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC ya kuwataka
wajiengue kwenye kinyang'anyiro hicho cha urais. Kutokana na kuibuka
mivutano hiyo, uchaguzi wa rais nchini humo uliopangwa kufanyika Julai
24, sasa utafanyika Agosti 23 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment