24Rajab,1434
Hijiriyah/ JUNY 03,2013 Miyladiyah
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard
Membe amesema kuwa, kamwe Tanzania haitaiomba radhi Rwanda, baada ya
Rais Jakaya Kikwete kuishauri nchi hiyo kufanya mazungumzo na upinzani
ili kumaliza vita katika eneo la Maziwa Makuu. Serikali ya Rwanda
ilikuwa imeitaka Tanzania iombe radhi kwa madai kuwa kauli ya Rais
Kikwete ni kama tusi kwao na kwamba wao hawawezi kukaa na kuzungumza na
wapinzani ambao ni wauaji. Membe amesema kama ninavyomnukuu: “Kama
Rwanda haitaki kufuata ushauri wa Rais Kikwete inatakiwa kuuacha na siyo
kumtaka aombe radhi,” mwisho wa kunukuu. Membe aliyasema hayo jana
alipokuwa akitoa ufafanuzi huo bungeni. Tamko hilo la Serikali ya
Tanzania limekuja ikiwa zimepita takriban siku sita tangu serikali ya
Rwanda itowe tamko la kupinga ushauri huo uliotolewa na Rais Kikwete
wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa
Afrika (AU), uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment