Bajeti za nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilitangazwa jana zikitoa vipaumbele katika masuala ya usalama, afya, kilimo, elimu, nishati na kuboresha miundombinu.
Bajeti hizo zilizotangazwa na mawaziri wa fedha wa
nchi hizo sambamba na ile ya Tanzania, ni za Uganda, Rwanda na Kenya
ambayo iliongoza kwa ukubwa wa bajeti.
Bajeti hizo zilitofautiana kwa kiasi kikubwa kutokana na mahitaji na vyanzo vya mapato kwa kila nchi.
Mwelekeo wa bajeti hizo pia umelenga kuongeza
mapato kupitia vyanzo vya ndani kwa kuongeza ushuru na kodi kwenye
vileo, vyombo vya usafiri na bidhaa za anasa.
Kenya Sh28.5 trilioni
Waziri wa Fedha wa Kenya, Henry Rotich alisema
kwamba Bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2013/14 itafikia Sh1.5
trilioni za Kenya (sawa na Sh28.5 trilioni za Tanzania).
Bajeti hiyo ilisomwa jana bungeni jijini Nairobi, ndiyo ya kwanza kwa Rais Uhuru Kenyatta aliyechukua madaraka hivi karibuni.
Moja ya ameneo muhimu yaliyopewa kipaumbele katika
bajeti hiyo ni elimu, ambapo Sh17.4 bilioni (Sh330.6 bilioni za
Tanzania) zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha mkakati wa Serikali ya
Jubilee wa kununua kompyuta ndogo 1,300,000 kwa ajili ya wanafunzi wa
shule za msingi.
Uganda Sh7.2 trilioni
Waziri wa Fedha wa Uganda, Maria Kiwanuka
ametangaza Bajeti ya Serikali ya nchi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2013/14
ambapo ambapo Sh 12 trilioni (sawa na Sh7.2 trilioni za Tanzania)
zitatumika.
Bajeti hiyo inategemea vyanzo vya ndani vya mapato
baada ya misaada ya wafadhili kushuka kwa zaidi ya asilimia 93, kutoka
Sh749 bilioni (za Uganda) mwaka 2012/13 hadi Sh50 bilioni za Uganda
mwaka 2013/14.
Kiwanuka alisema katika mwaka huu wa fedha,
wafadhili wamesaidia asilimia 25 ya bajeti ya nchi hiyo lakini katika
mfumo wa mikopo na kufadhili miradi, ambapo matumizi ya Serikali
yatafikia Sh8.4 trilioni za Uganda.
0 comments:
Post a Comment