Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 27 June 2013

Kasi ya ugonjwa wa kisukari yaongezeka nchini




Serikali imesema ugonjwa wa kisukari umeenea kwa kati ya asilimia 0 hadi 20 katika wilaya 50 za Tanzania Bara.

Takwimu hizo zilitolewa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashidi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mgogoni, Kombo Khamis Kombo (CUF).

Mbunge huyo alitaka kujua kama serikali imefanya utafiti wa ugonjwa wa kisukari ambao unapoteza maisha ya wananchi wengi.

Pia, alihoji kama serikali imetoa elimu gani kwa wananchi ili kuepuka magonjwa nyemelezi yanayosababishwa na ugonjwa huo.

Dk. Rashidi alisema tafiti zilizofanyika miaka ya 1986/87 na baadaye mwaka 1996/97 katika mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mara na Mwanza, zilionyesha kuwa ugonjwa wa kisukari ulikuwa umeenea kwa asilimia moja vijijini na asilimia tatu jijini Dar es Salaam.

Alisema mwaka 2005, idadi hiyo ilikuwa imefikia asilimia tano kwa wakazi wa Dar es Salaam.

“Utafiti wa viashiria vya magonjwa yasiyoambuzika kwa nchi nzima umeonyesha kuwa ugonjwa wa kisukari umeenea kati ya asilimia 0 hadi 20 katika wilaya 50 za Tanzania Bara,” alisema.

Aidha, alisema matokeo ya utafiti huo yatasaidia kubuni mbinu za kudhibiti vichochezi vinavyosababisha ongezeko la ugonjwa huo na magonjwa yasiyoambuzikiza nchini.

Kuhusu kutoa elimu, alisema serikali inafahamu kuwa elimu ni kiungo muhimu katika kuongeza uelewa wa jamii kuhusu magonjwa mbalimbali.

“Elimu juu ya ugonjwa wa kisukari na elimu ya afya hutolewa kwenye hospitali mbalimbali na vituo vya kutolea huduma za afya nchini,” alisema



0 comments:

Post a Comment