Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 27 June 2013

Zaidi ya Sh. bilioni 100 zatengwa kununua chakula cha akiba




Wakala Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imetengewa Sh. bilioni 110.4 kwa ajili ya kununua tani 235,000 za mahindi na tani 15,000 za mtama kutoka kwa wakulima.

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima aliliambia Bunge jana kuwa, katika mwaka wa fedha 2013/14 wakala huo pia utanunua takribani tani 50,000 za mahindi kutoka mkoa wa Ruvuma ikiwamo Jimbo la Peramiho.

“Kutokana na mabadiliko ya mfumo na utaratibu wa bajeti ya serikali, ni matarajio ya wizara yangu kuwa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ununuzi wa mazao ya wakulima utawahi msimu wa mavuno kutoka maeneo mbalimbali nchini ili kuwezesha mazao ya wakulima kununuliwa kwa wakati,” alisema.

Malima alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM), ambaye alitaka kujua utaratibu gani uliopangwa katika ununuzi wa mahindi.

Pia, alihoji ni kiasi gani cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya ununuzi wa mahindi katika Jimbo la Peramiho, wilaya ya Songea.

0 comments:

Post a Comment