Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 22 June 2013

GE, Symbion kuzalisha umeme wa gesi Mtwara

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.  
 Kampuni za GE Africa na Symbion Power Tanzania, zimeingia mkataba wa kutekeleza kwa pamoja mradi wa kuzalisha megawati 400 za umeme wa gesi mkoani Mtwara.
Umeme wa mradi huo utasambazwa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na mikoa mingine nchini na utaanza mwaka 2017.
Makubaliano ya ushirikiano huo, yalisainiwa jana mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Mkataba huo ulisainiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa GE Africa, Jay Ireland na Meneja Mkuu wa Symbion Power Don Brindle.
Makubaliano hayo yatahusisha pia ujenzi wa njia za umeme kutoka Mtwara hadi Songea mkoani Ruvuma na uzalishaji wa megawati 200 za awali zitaanza mwaka 2017.
Mkataba pia utahusu ujenzi wa Kiwanda cha Saruji mkoani Mtwara kitakachogharimu Dola za Marekani 500 milioni.
“Tumeingia mkataba na Symbion wa kuongeza nguvu katika jitihada kuwekeza katika sekta ya umeme na gesi asili na tutasaidiana nao katika masuala ya kiufundi na maendeleo, uhandisi, fedha na maeneo mengine,” alisema Mtendaji Mkuu wa GE Africa.
Kwa upande wake, Waziri Muhongo alisema kiwanda cha saruji kitakachojengwa mkoani Mtwara kitakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 300 milioni kwa mwaka.
Katika mazungumzo yake, aliwapuuza wanaopinga Mradi wa Kusafirisha Gesi kutoka Mtwara kwendea Dar es Salaam kwa njia ya bomba.
Waziri huyo alisisitiza kuwa bidhaa lazima zifike sokoni.
“Mahindi, matunda na bidhaa nyingine zinaletwa Dar kwa kuwa ndiyo kwenye soko sasa vipi gesi,” alihoji Muhongo na kuongeza kuwa kupitia gesi asili, Tanzania inataka kuuza nje ya nchi umeme, hatua ambayo itasaidia katika ukuaji wa pato la Taifa.
 

0 comments:

Post a Comment