Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday 30 June 2013

Ehab Fahmy: Mursi yuko tayari kwa mazungumzo

                                  22 shaaban,1434 Hijiriyah/ 01 july,2013 Miyladiyah

 


Msemaji wa Rais Muhammad Mursi wa Misri amesema kuwa, mazungumzo ndiyo njia pekee ya kuiepusha nchi hiyo na mgogoro wa kisiasa. Ehab Fahmy amefafanua kuwa, ikulu ya rais imejiandaa kufanya mazungumzo ya kitaifa na ya kweli. Aidha Ehab amewataka wapinzani kufanya maandamano ya amani. Kwa upande mwingine msemaji huyo wa rais ametangaza kuwa, Rais Muhammad Mursi amekiri kufanya baadhi ya makosa na kuahidi kuyarekebisha. Rais Mursi amenukuliwa akisema kuwa, Misri haitoshuhudia mapinduzi mengine wala uchaguzi wa mapema. Mursi ameyasema hayo, alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari wa gazeti la The Guardian na kuwataka wapinzani wake, kuacha maandamano. Hii ni katika hali ambayo mamilioni ya Wamisri wenye hasira wanaendelea kufanya maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakimtaka Rais Muhammad Morsi ajiuzulu na kuitisha uchaguzi wa kabla ya wakati. Katika upande mwingine, maelfu ya wafuasi wa Morsi nao wameandamana wakimtaka rais huyo aendelee kusalia madarakani kwa hoja kuwa amechaguliwa kihalali na wananchi.

0 comments:

Post a Comment