Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon na Rais Muhammad Mursi wa
Misri, wamesisitizia haja ya kutatuliwa mgogoro wa Syria kwa njia za
kisiasa. Habari zinasema kuwa, viongozi hao wamefikia makubaliano hayo
kupitia njia ya simu sambamba na Ban Ki moon kushukuru juhudi za
kidiplomasia zinazofanywa na Cairo kuhusiana na kadhia ya Syria. Aidha
mazungumzo hayo yalijalidi hali ya Syria na kuitaka jamii ya kimataifa
kuchukua hatua za lazima za kukomesha umwagaji damu nchini humo na
kuanza mchakato wa kisiasa wa kutatua mgogoro huo. Kwa mujibu wa ripoti
hiyo, Rais Muhammad Mursi, amesisitizia udharura wa kuharakishwa mkutano
wa Geneva 2 na kuongeza kuwa, Cairo itawasilisha mtazamo wake katika
kikao hicho. Ban Ki moon na Rais Mursi wa Misri pia wamezungumzia ripoti
ya Tume ya Pande Tatu inayofuatilia na kuchunguza athari za ujenzi wa
bwawa la an-Nahdha la Ethiopia ambapo Rais Musri alisisitiza kuwa, Misri
yenye uchumi mzuri zaidi kati ya nchi nchi zinazopakana na mto Nile,
italinda maslahi ya nchi za jirani kwa sharti Cairo isiathiriwe na
matumizi ya nchi nyingine ya maji ya mto huo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment