Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 15 June 2013

Zaidi ya asilimia 70 washiriki uchaguzi mjini Tehran

                               
 
Mjumbe moja wa Kamati ya Utendaji ya Kituo cha Uchaguzi nchini Iran amesema kuwa, hadi anatangaza habari hiyo, zaidi ya asilimia 70 ya watu waliotimiza masharti ya kupiga kura mjini Tehran walikuwa tayari wameshiriki katika duru ya 11 ya uchaguzi wa rais na duru ya nne ya uchaguzi wa mabaraza ya miji na vijiji hapa nchini.
Bw. Ismail Kauthari ameongeza kuwa wanatabiri kuwa asilimia 70 ya wananchi wa Tehran wamejitokeza kupiga kura huku idadi kubwa zaidi ya watu waliopiga kura ikiwa ni ya wananchi wa mikoani na vijijini.
Hadi tunapokea habari hii, upigaji kura ulikuwa bado unaendelea na ulikuwa tayari umeshaongezewa muda kwa mara kadhaa jambo ambalo linaonesha wazi kuwa asilimia ya watu walioshiriki kwenye zoezi hili muhimu itakuwa zaidi ya hiyo.

0 comments:

Post a Comment