Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 5 May 2013

Wanajeshi saba wa Markeani wauawa Afghanistan


Wanajeshi saba wa Marekani wanaohudumu katika kikosi cha NATO wameuawa katika matukio mawili nchini Afghanistan.
Ripoti zinasema wanajeshi watano wameuawa katika mkoa wa Kandahar kusini mwa Afghanistan wakati gari lao la deraya lilipolipuliwa kwa bomu la kutegwa barabarani. Mkuu wa polisi Kandahar amesema tukio hilo lilijiri Jumamosi saa sita mchana katika wilaya ya Maiwand. Masaa machache baadaye askari wa Jeshi la Afghanistan aliwafyatulia risasi na kuwaua wanajeshi wawili wa Mareknai katika mkoa wa Farah magharibi mwa nchi hiyo. Wanamgambo wa Taliban wamesema mfuasi wao alijipenyeza katika jeshi la Afghanistan na kutekeleza hujuma hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya icasualties.org hadi sasa wanajeshi 3,299 wa kigeni wameuawa Afghanistan tokea Marekani iongoze uvamizi dhidi ya nchi hiyo Oktoba mwaka 2001. Aghalabu ya wanajeshi waliouawa ni kutoka Marekani.

0 comments:

Post a Comment