Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 9 May 2013

Vita dhidi ya kutumiwa watoto vitani vyaanza Congo



Jumuiya moja isiyo ya kiserikali imeanzisha mapambano dhidi ya kutumiwa watoto wadogo vitani huko kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) nchini Congo umetangaza kuwa watoto wengi wamekuwa wakitumiwa vitani na makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha kusini magharibi mwa Congo. UNICEF imesisitiza kuwa makundi ya wanamgambo yanatumia imani za kijadi kuwachochea watoto hao na kuwadanganya kwamba hawawezi kuuawa kwa kupigwa risasi jambo ambalo linawatumbukiza wengi katika makucha ya mauti.
Ripoti zinasema makundi ya wanamgambo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanakusanya vijana wenye umri mdogo kwenye kwenye vijiji vya nchi hiyo kwa ahadi ya kuwapa elimu na kuwatumia katika vita. UNICEF imesema watoto zaidi ya 1500 wamekuwa wahanga wa makundi hayo huko kusini magharibi mwa Congo.
 

0 comments:

Post a Comment