Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 7 May 2013

Ujenzi Barabara ya Mwenge-Tegeta wachelewa kukamilika

Ujenzi wa barabara ya Bagamoyo kuanzia Mwenge hadi Tegeta jijini Dar es Salaam umekwama kumalizika kama ilivyopangwa huku baadhi ya vifaa vya kazi vikiwa vimeondolewa eneo la mradi.

Uchunguzi  umebaini kuwa vifaa muhimu kama magari, matrekta na  vijiko vya kuchimbia mitaro havionekani barabarani

Aidha, ujenzi wa madaraja uliokuwa unaendelea katika barabara hiyo nao umesimama kwa kipindi kirefu huku msongamano wa magari ukiwa unazidi kuongezeka kutokana na barabara moja kufungwa.

Awali wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo ambao ulifanywa na Rais Jakaya Kikwete, serikali iliahidi kukamilisha ujenzi huo Mei mwaka huu ili kurahisisha suala la usafiri kati ya Mwenge hadi Tegeta.

Hata hivyo, alipoulizwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale, alisema serikali iliongeza muda wa kukamilisha ujenzi huo ingawa hakutaka kufafanua zaidi.

Mfugale alikanusha madai kwamba ujenzi huo umekwama na kwamba kinachofanywa na mkandarasi hivi sasa ni kujenga taratibu ili barabara iweze kuwa imara zaidi.

Aliongeza kuwa serikali haitaki kupokea barabara mbovu na kwamba wanafuatilia ili kuona kazi hiyo inakamilika kwa mujibu wa mkataba mpya waliongeza kwa mkandarasi huyo.

0 comments:

Post a Comment