Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 2 May 2013

Serikali ya Chad yazima jaribio la mapinduzi

Serikali ya Chad imetangaza kuwa imezima jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali na kuwatia mbaroni waliohusika.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Chad imeeleza kwamba, jana Jumatano Mei Mosi 'kikundi kidogo' cha watu waliokuwa na fikra mbaya kilikusudia kufanya mapinduzi ya kijeshi na kupindua serikali lakini jaribio hilo limezimwa. Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa, wafuasi wa kundi hilo pia kwa miezi minne iliyopita wamekuwa wakifanya njama za kuhatarisha amani ya Chad, na kwamba waliopanga mpango huo wametiwa mbaroni na wanachunguzwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo serikali ya Chad haikutoa maelezo zaidi kuhusiana na kundi hilo ingawa jeshi limesema kuwa waliokamatwa ni askari na raia wa kawaidia akiwemo Saleh Makki, mbunge wa mrengo wa upinzani.

0 comments:

Post a Comment