Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 2 May 2013

M23 yasimamisha mazungumzo na Kinshasa


Harakati ya waasi ya M23 imesema kuwa imesimamisha mazungumzo na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na Umoja wa Mataifa kuidhinisha kikosi cha kupambana na waasi mashariki mwa Kongo. Rene  Abandi, kiongozi wa ujumbe wa M23 katika mazungumzo na serikali ya Kinshasa yanayofanyika nchini Uganda amesema, mwenendo wa mazungumzo hayo umeingia doa kutokana na Umoja wa Mataifa kupeleka kikosi cha kupambana na waasi, na kwamba wana matumaini serikali ya Kongo DRC itaelewa baadaye kwa nini vita haviwezi kutatua mgogoro wa mashariki mwa nchi hiyo. Waasi hao pia wamesema kuwa, wanakisubiri kwa hamu kikosi hicho na kwamba wako tayari kupambana nacho.
Hii ni katika hali ambayo, kikosi kipya cha jeshi la UN kinatarajiwa kuwasili hivi karibuni Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

0 comments:

Post a Comment