02,RAJAB,1434 Hijiriyah/ May 12,2013 Miyladiyah
Mwanasheria Mkuu wa Kenya amejiweka mbali na ombi la balozi na
mwakilishi wa kudumu wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa aliyelitaka
Baraza la Usalama la umoja huo lisimamishe kesi zinazowakabili Rais
Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika Mahakama ya Kimataifa
ya Jinai ICC.
Githu Muigai Mwanasheria Mkuu wa Kenya amenukuliwa leo
akisema kuwa, serikali ya nchi hiyo haina taarifa na barua kama hiyo
katika Umoja wa Mataifa na kwamba, huo sio msimamo rasmi wa serikali ya
Nairobi.
Githu Muigai ameongeza kuwa, msimamo rasmi wa serikali ya Kenya
ni kushirikiana kikamilifu na Mahakama ya Kimataifa na kwamba, Nairobi
ina lengo la kuendeleza ushirikiano huo
. Hayo yanajiri katika hali
ambayo, wakili wa William Ruto juzi alitangaza kwamba, mteja wake
hafanyi juhudi za kutaka kusitishwa kesi inayomkabili katika Mahakama ya
Kimataifa ya Jinai ICC.
Ikumbukwe kuwa, siku ya Alkhamisi Macharia
Kamau Mwakilishi wa Kudumu wa Kenya katika Umoja wa Mataifa aliwasilisha
barua katika Baraza la Usalama la umoja huo akitaka kusimamishwa kesi
dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika Mahakama
ya Kimataifa ya Jinai ICC.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment