Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 2 May 2013

Iran yalaani mashambulizi ya Mabudha wa Myanmar


                                23Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ May 03,2013 Miyladiyah
 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mashambulizi yanayofanywa na genge la Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu nchini Myanmar na kuharibiwa misikiti pamoja na makazi ya Waislamu hao.
Ramin Mehmanparast ameelezea kusikitishwa kwake na machafuko hayo na kusema kuwa, kuendelea vitendo hivyo vya kikatili na visivyo vya kibinadamu nchini Myanmar dhidi ya Waislamu ni jambo lenye kutia wasiwasi. Amesisitiza udharura wa kukabiliana ipasavyo na wahusika wa vitendo hivyo na kusema kuwa, ana matumaini serikali ya Myanmar itashirikiana na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na makundi mengine ili kuzuia kukaririwa vitendo kama hivyo vya kushambuliwa Waislamu nchini humo.
Siku ya Jumanne iliyopita mtu mmoja aliuawa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya genge la Mabudha kuchoma moto maelfu ya nyumba za Waislamu na kukalia kwa mabavu misikiti miwili kwenye eneo la Okkan katikati mwa Myanmar.

0 comments:

Post a Comment