Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 2 May 2013

Waasi wa FLEC nchini Angola wabadili msimamo

                        23Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ May 03,2013 Miyladiyah
 Waasi wa kundi linalopigania kujitenga eneo la Cabinda nchini Angola FLEC wamesema wako tayari kuweka silaha chini na kuzungumza na serikali ya nchi hiyo. Waasi hao wamesema mazungumzo yoyote kati yao na serikali sharti yatilie maanani kilio cha miaka mingi cha wakaazi wa eneo hilo. FLEC imekuwa ikipigania kujitenga eneo hilo lililoko kaskazini mwa mji mkuu wa Angola, Luanda kwa miongo kadhaa sasa. Cabinda ni eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta lakini wakaazi wake wanaishi katika hali mbaya ya umasikini. Kundi la FLEC lilitangaza kusitisha vita mwaka 2006 dhidi ya serikali ya Angola lakini hadi sasa limekuwa likifanya mashambulizi ya kuvizia. Itakumbukwa kuwa, mwaka 2010 kundi hilo lilishambulia timu ya taifa ya Togo ilipokuwa ikielekea Angola kushiriki mashindano ya soka ya mataifa bingwa barani Afrika.

0 comments:

Post a Comment