KUFUATIa mauaji ya
kishirikina yaliyoibuka kwa kasi Mkoani Mbeya
hivi karibuni ,MKUU wa Wilaya ya Chunya ,Bw.
Deodatusi Kinawiro amewataka Madiwani wa halmashauri hiyo kukemea
maovu hayo ambayo yameanza kuonyesha
sura mbaya ya wilaya hiyo kwa watu wa nje.
Hatua hiyo inafuatiwa
na mauaji hayo kushamili mwishoni mwa wiki katika kata ya
Mwajuni mtaa wa Maweni kwa kikonge
mmoja ambaye alikuwa mzee wa kanisa kuuwawa kwa imani za
kishirikina kisha kufukiwa kaburi moja na marehemu
baada ya kutuhumiwa kumroga kijana mmoja kijijini hapo.
Bw. Kinawiro aliyasema hayo
jana wakati akizungumza na mtandao huu kuhusiana na mauaji ya kishirikina
yaliyoshamiri Wilayani humo na
kuanza kuwatua hofu wananchi wanaotoka maeneo mbali
mbali ya mikoa jirani kwa ajili ya kutafuta
maisha.
“Kwa ujumla hivi
sasa wilaya imekuwa na viashirio vya mauaji
mengi sana yanayohusisha ushirikina wa ajabu
, ulevi wa kupita kiasi ambao
unasababisha vifo vingi sana katika wilaya mfano huyu mzee
mstaafu wa kanisa aliyeuwawa hivi karibuni kwa visa
tu na kuanza kumtuhumu uchawi kwa kuanza kumpiga mawe na kisha
kumzika kaburi moja na marehemu “alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo Bw. Kinawiro
aliwataka madiwani kuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha kuwa wanatemvelea katika kata zao na kuongea na
wananchi kuelimisha madhara ya kuamini ushirikina ambayo mpaka sasa yamekuwa
kero kubwa na hqata kuwafanya wananchi waishi kwa hofu
.
“Mi nashangaa sana
kwanini wananchi wawe na imani potofu kiasi
hiki kwanini isijulikane kuwa mtu
ameumwa ugonjwa wa maralia lakini nashangaa sana kuona
wananchi wakimbilia uchawi, hii haivumiliki hata kidogo vinginevyo hali
hii ikiendelea kutakuja kutokea maafa makubwa”alisema Mkuu huyo.
Mkuu huyo wa Wilaya aliendelea na kuongeza
kuwa madiwani walio wengi wapo karibu na
wananchi kiasi kwamba wana uwezo mkubwa wa kuhakikisha hili
linakwisha na kurudisha amani kwa wananchi
na watu wengine wa nje.
Aidha Bw.Kinawiro aliwalaumu Makatibu
tarafa kwa tabia zao za kukaa kimnya na taarifa za
migogoro ambazo zimekuwa zikitokea na hivyo
baadae kutokea vifo wakati uwezekano wa kulitafutia
ufumbuzi ulikuwepo.
Mwisho.
"Chanzo Francis Godwin"
0 comments:
Post a Comment