Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 16 May 2013

CUF yateua mgombea Chambani 

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemteua Yusuph Hussein kuwa mgombea ubunge wa chama hicho katika jimbo la Chambani- Pemba, mjini Zanzibar.
Uteuzi huo umefanyika na kikao cha Baraza la Kuu la Uongozi la Taifa kilichofanyika Mei 14 na 15 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa chama hicho kitaifa, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema baraza hilo limewataka wananchi wa jimbo hilo kuitumia nafasi hiyo ili kuleta mabadiliko ya kisiasa kwa kukiunga mkono chama hicho na mgombea wake katika uchaguzi utakaofanyika Juni 16, mwaka huu.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka 2010, Salim Hemed (marehemu), alishinda kwa asilimia 84 pamoja na kuwepo uchakachuaji wa kura, hivyo kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano huohuo katika kumpata mbunge.
Akizungumzia mchakato wa Katiba mpya, alisema rasimu itakayoandaliwa iwekwe hadharani kwa wakati, ili wananchi waweze kutoa maoni yao kabla haijapelekwa katika Bunge la Katiba na kupigiwa kura na wananchi.
“CUF haitakuwa tayari kuiunga mkono Katiba ambayo haitakuwa na misingi imara ya kidemokrasia na isiyotokana na maoni ya Watamzania; tutakuwa tayari kuwahamasisha Watanzania nchi nzima kuikataa Katiba isiyotokana na maoni yao,” aliongeza.

0 comments:

Post a Comment