Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 28 May 2013

Australia yapunguza vikwazo dhidi ya Zimbabwe

Serikali ya Australia imetengua baadhi ya vikwazo ilivyoviweka dhidi ya baadhi ya viongozi wa Zimbabwe. Bob Carr Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Australia amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo imefuta vikwazo ilivyoviweka dhidi ya shakhsia 65 wa Zimbabwe wakiwemo viongozi wa ngazi za juu wa serikali na wa kijeshi wa nchi hiyo. Bob Carr ameongeza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa baada ya serikali ya Harare kukamilisha zoezi la uundwaji wa katiba mpya, ambayo ni chachu ya kufanyika mabadiliko kwenye muundo wa utawala nchini humo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, wajumbe wa Bunge la Seneti la Zimbabwe tarehe 14 Mei waliipitisha rasimu ya katiba mpya na kutiwa saini baadaye na Rais Robert Mugabe tarehe 22.

0 comments:

Post a Comment