Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 28 May 2013

Raia 25 wauliwa Jamhuri ya Afrika ya Kati


Watu wasiopungua 25 wameuawa baada ya wanamgambo wa Muungano wa Seleka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kushambulia vijiji kadhaa katika mji wa Bossangoa ulioko magharibi mwa nchi hiyo. Taarifa zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu zinasema kuwa, miongoni mwa waliouawa ni wanawake na watoto wadogo. Wanamgambo wa Seleka ambao hivi sasa wanashikilia  uongozi wa nchi hiyo, wanatuhumiwa kutenda vitendo kadhaa za jinai ikiwa ni pamoja na uporaji wa mali, mauaji, ubakaji na unyanyasaji wa raia. Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu yanasema kuwa, mara baada ya wanamgambo wa Seleka kumuondoa madarakani Rais Francois Bozize tarehe 24 Machi mwaka huu, hali ya amani na utulivu imetoweka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

0 comments:

Post a Comment