Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 27 April 2013

Waziri Mkuu wa Iraq atoa wito wa umoja




Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki ametoa wito kwa Waislamu Iraq kudumisha umoja na kusema machafuko ya kimadhehebu nchini humo yameibuliwa na watu wanaopata himaya kutoka nchi za kigeni.
Maliki ameyasema hayo siku ya Jumamosi alipohutubua Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu ambalo limefanyika katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Watu zaidi ya 200 wameuawa katika wimbi jipya la machafuko ambalo lilianza Iraq Jumanne iliyopita.
Waziri Mkuu wa Iraq ametoa wito kwa wasomi wa Kiislamu wanaoshiriki katika kikao hicho kujaribu kutafuta sulushisho la machafuko ya Iraq.
Al Maliki amezituhumu nchi jirani za Saudi Arabia na Qatar kuwa ndio chanzo cha uchozezi wa machafuko ya kimadhehebu nchini humo.



0 comments:

Post a Comment