Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 27 April 2013

‘Iran inaweza kuwa na nishati ya nyuklia bila vikwazo’




Mgombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao wa Iran Dkt. Ali Akbar Velayati amesema mgogoro kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran unaweza kutatuliwa ili nchi hii inufaike na nishati ya nyuklia pasina kuwepo vikwazo.
Velayati ameongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa ni dola lenye nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa hivi sasa hakuna suala lolote linaloweza kutatuliwa kieneo pasina kuhusihwa Iran jambo ambalo linaashiria ushawishi mkubwa wa nchi hii. Velayati ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje hivi sasa ni mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Amesema kukiwepo usimamizi bora, Iran inaweza kuchukua nafasi ya kwanza kiuchumi katika eneo ifikapo mwaka 2025. Velayati ameunda muungano na wanasiasa vigogo wanaofungamana na misingi ya mapinduzi ambao ni spika wa zamani wa bunge Dkt. Gholam-Ali Haddad Adel na meya wa Tehran Mohammaed-Baqer Qalibaf. Muungano huo utamteua moja kati yao ambaye ataongoza katika kura za maoni ili ashiriki katika uchaguzi wa atakaye chukua nafasi ya Rais Mahmoud Ahmadinejad amabaye amemaliza mihula miwili ya kikatiba. Uchaguzi wa 11 wa rais wa Iran utafanyika Juni 14 na zaidi ya wagombea 21 wametangaza nia kuwa kuwania nafasi ya urais.


0 comments:

Post a Comment