Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 26 April 2013

Watu 25 wauawa katika mapigano mapya Nigeria
Mapigano mapya yaliyozuka kati ya askari usalama wa Nigeria na kundi la wanamgambo wa Boko Haram huko katika kijiji cha Jashwa kilichopo katika jimbo la Yobe kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, yamepelekea kuuawa watu wasiopungua 25.
Mkuu wa polisi katika jimbo la Yobe Alhaji Sanusi Rufai amesema kuwa, kati ya watu hao waliouawa ni pamoja na wanamgambo 20 wa Boko Haram na askari 5 na kwamba, askari wengine wawali wamejeruhiwa na kulazwa hospitali. Sanusi amesema kuwa, wanamgambo hao walivamia nyumba ya kiongozi wa benki moja iliyopo jimboni hapo na kuiba pesa zote zilizokuwemo.
Wakati huo huo, msemaji wa polisi ya Nigeria amesema kuwa, katika mapigano hayo askari usalama wa nchi hiyo wamefanikiwa kudhibiti aina mbalimbali za silaha na mabomu ya kurusha kwa mkono na magari matatu vilivyokuwa vikidhibitiwa na wanamgambo hao.

0 comments:

Post a Comment