Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday 26 April 2013

Al-Marzouqi: Hali ya hatari lazima ifutwe Tunisia




Rais Munsif Al Marzouqi wa Tunisia amesema kuwa, umewadia wakati wa kufutwa hali ya hatari liyoanza kutekelezwa mwaka 2011 nchini humo. Akiashiria kwamba, kutekelezwa hali hiyo ya hatari nchini kumegharimu kiasi kikubwa cha nguvu kazi na fedha nyingi Rais wa Tunisia amesema, lazima hali hiyo ifutiliwe mbali ili askari waweze kutekeleza majukumu yao asili.
Itakumbukwa kuwa, mwanzoni mwa mwaka huu, Tunisia ilirefusha hali ya hatari kwa kipindi kingine cha miezi mitatu hadi mwezi Juni. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, kunapotokea hatari inayotishia usalama wa nchi au tukio lolote la hatari, kunapaswa kutangazwa hali ya hatari nchi nzima au katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika

0 comments:

Post a Comment