21,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 03,2013Miyladiyah
Watu 13 wamefariki dunia kutokana na moto ulioteketeza shule ya Waislamu
nchini Myanmar. Moto huo uliotokea leo katika mji wa Yangon nchini
humo, umezusha hasira kali kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na serikali
kushindwa kudhibiti vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa dhidi ya
Waislamu, licha ya ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa na watawala wa nchi
hiyo za kukabiliana na wahalifu. Aidha habari zaidi zinasema kuwa,
wakati moto huo ukitokea katika shule hiyo iliyokaribu na msikiti, zaidi
ya watu 70 walikuwa wamelala. Polisi imetangaza kuanzisha uchunguzi
katika tukio hilo huku ikidai kuwa, huenda moto huo ulisababishwa na
hitilafu ya umeme. Kutokana na kuongezeka vitendo vya jinai dhidi ya
Waislamu wa Myanmar, Jamii ya Waislamu wa nchi hiyo inaishi katika hali
ya wasiwasi na hofu kubwa. Hii ni katika hali ambayo, jumuiya za
kimataifa zimeendelea kufumbia macho jinai hizo. Kufuatia hali hiyo,
Sheikh Abdul Alim Mussa imam wa msikiti wa al-Islam wa mjini Washington,
Marekani hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa, nchini Myanmar
kunaendelea vita vya dunia dhidi ya Waislamu huku Umoja wa Mataifa ukiwa
umenyamaza kimya.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment