Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 18 April 2013

Wamisri waandamana kupinga hukumu ya Mubarak




Familia za mashahidi waliouawa wakati wa harakati za mapinduzi nchini Misri mwaka 2011 zimeandamana kupinga hukumu ya mahakama iliyotolewa kuhusiana na diktetea aliyepinduliwa nchini humo Hosni Mubarak.
Maandamano hayo yamefanyika baada ya mahakama ya Misri kuamua kuwa, kifungo cha Mubarak kutokana na kuuawa waandamanaji hakitaendelea eti kwa kuwa tayari amekuwa kizuizini kwa karibu miaka miwili sasa.
Hata hivyo mahakama hiyo imeamua kuwa atarudishwa korokoroni akisubiri kesi inayohusu udanganyifu.
Mahakama ya Misri imeamuru diktetea Hosni Mubarak arejeshwe jela kutoka katika hospitali ya kijeshi alikokuwa akitibiwa baada ya afya yake kuwa nzuri.

Waandamanaji hao wamepinga hukumu hiyo na kutaka mwendesha mashtaka mkuu ajiuzulu na dikteta huyo anyongwe.

Itakumbukwa kuwa mwezi Juni mwaka jana Hosni Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya kuuawa karibu waandamanaji 900 wakati wa harakati za mapinduzi nchini Misri zilizomng'oa madarakani.


0 comments:

Post a Comment