Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 18 April 2013

Jonathan aunga mkono kusamehewa Boko Haram









Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ameunda kamati mpya ya kuangalia namna ya kusamehewa kundi la waasi la Boko Haram.
Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya rais huyo, kamati hiyo itatekeleza mwenendo huo wa msamaha kwa siku 60 katika fremu ya mazungumzo na kupokonywa silaha wafuasi wa kundi hilo.
 Pia imeelezwa kuwa, kamati hiyo ya Rais wa Nigeria inayoundwa na wajumbe 25 wakiwepo wanajeshi, wasomi na wanasiasa itajaribu kuielimisha jamii sababu zinazopelekea uasi ili kuzuia waasi kama hao kutokea tena nchini humo.
Vilevile Rais Jonathan ameamuru kuundwa kamati nyingine itakayoshughulikia suala la silaha ndogo ndogo ili kuimarisha usalama na kupunguza ukosefu wa amani. 
Wito wa kusamehewa kundi la Boko Haram ulitolewa hivi karibuni na viongozi wa kidini na kisiasa wa kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mashambulizi na uasi wa kundi hilo umesababisha maelfu ya watu kuuawa nchini humo tangu mwaka 2009.


0 comments:

Post a Comment