Serikali ya Sudan imeionya
Marekani na propaganda zake chafu za kisiasa dhidi ya Khartoum na
kusisitiza kwamba, hatua ya Washington ya kuwataka Wamarekani
wajihadhari na kufanya safari nchini Sudan ni ya kisiasa. Taarifa ya
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan imesisitiza kwamba, tangazo hilo
la Marekani lina malengo na matashi ya kisiasa. Abubakar Siddiqi,
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan amesema kuwa, tahadhari
hiyo ya Marekani sio jambo jipya.
Jana Wizara ya Mashauri ya
Kigeni ya Marekani iliwataka raia wake wajihadhari kufanya safari nchini
Sudan hususan katika maeneo yanayokabiliwa na machafuko ya jimbo la
Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile. Hata hivyo viongozi wa Khartoum
wameitathmini tahadhari hiyo kwamba, ni muendelezo wa siasa chafu za
Marekani dhidi ya Sudan. Hivi karibuni viongozi wa Sudan walisisitiza
kwamba, viongozi wa Magharibi hususan wa Marekani wamekuwa wakifanya
njama za kuonyesha kwamba, nchini Sudan hakuna amani ili kwa njia hiyo
waweze kunufaika kisiasa na jambo hilo.
0 comments:
Post a Comment