Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 25 April 2013

Uhuru aendelea kutangaza majina ya mawaziri wapya

                

 Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta mapema leo ametangaza majina zaidi ya watu anaowapendekeza kuwa mawaziri kwenye serikali yake mpya. Rais Kenyatta amewaarifisha watu 12 wengi wao wakiwa wataalamu. Hata hivyo wanasiasa mashuhuri kama vile Najib Balala na Charity Ngilu watapata nafasi ya kurudi kwenye baraza la mawaziri iwapo bunge litawaidhinisha. Wawili hao ambao wamewahi kuhudumu kama mawaziri katika serikali zilizopita wamependekezwa kuongoza wizara za Madini na Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya miji. Hata hivyo rais wa Kenya bado hajatangaza watu watakaoongoza wizara za Mambo ya Ndani na Leba ingawa ameahidi kutoa tangazo kuhusu suala hilo katika siku chache zijazo. Wakili mashuhuri na balozi wa zamani wa Kenya nchini Ufaransa, Raychelle Omamo anependekezwa kuongoza wizara muhimu ya ulinzi. Bi. Omamo anakuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia wadhifa huo katika historia ya Kenya.

0 comments:

Post a Comment