24,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 05,2013Miyladiyah
Bunge la Burundi hapo jana Jumatano lilipitisha kwa wingi wa kura sheria
inayolenga kudhibiti sekta ya uandishi habari nchini humo. Sheria hiyo
inaipa uwezo serikali kumshurutisha mwanahabari kufichua vyanzo vyake
vya habari. Pia inapiga marufuku vyombo vya habari kutangaza au
kuchapisha habari kuhusu sarafu ya nchi, usalama wa taifa, wizara na
idara za ulinzi pamoja na kuikosoa safu ya juu ya uongozi wa nchi hiyo.
Siku moja baada ya sheria hiyo kupitishwa, lawama na ukosoaji
umejitokeza kutoka kila kona. Mwenyekiti wa chama cha wanahabari nchini
Burundi (UBJ), Bw. Alexandre Niyungeko amesema sheria hiyo inakiuka haki
muhimu ya kujieleza nchini humo. Ametoa wito kwa bunge kuwahusisha
wadau wote katika sekta ya uandishi habari ili papatikane sheria
inayokubalika na pande zote husika. Shirika la kimataifa la kutetea haki
za binadamu la Human Rights Watch kwa upande wake limelaani hatua ya
bunge la Burundi ya kupitisha sheria hiyo na kusema kuwa, serikali
inajaribu kuficha uozo katika safu za uongozi.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment